Lechantre amepania hasa, kuongeza dozi ya mazoezi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
12 Apr 2018
Lechantre amepania hasa, kuongeza dozi ya mazoezi Simba
Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema licha ya kupata matokeo mazuri, ataongeza dozi ya mazoezi katika kikosi hicho.

Kauli ya Lechantre imekuja siku moja baada ya Simba kuilaza Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kocha huyo mwenye CV ya kutinsha amesema ataongeza kasi na mbinu za mazoezi baada ya kuona ushindani wa kuwania ubingwa msimu huu ni mkali.

Mfaransa huyo alisema ushindani ni mkali, lakini ataongeza dozi kuwajenga vyema wachezaji wake kushindana na timu yoyote.

Lechantre alisifu juhudi za wachezaji wake katika kuipigania Simba kupata matokeo mazuri katika Ligi Kuu.

“Nawapongeza wachezaji wangu, wanaonyesha kweli wanataka ushindi katika kila mechi, wamekuwa wakifanya vizuri kwa kufuata maelekezo ingawa kuna makosa madogo,” alisema Lechantre.

Ushindi wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar umeongeza mchuano wa kuwania ubingwa msimu huu, baada ya Simba kufikisha pointi 52.

Simba, ambayo haijapoteza mchezo, inachuana na Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, ikiwania kurejesha mafanikio baada ya kukosa ubingwa kwa miaka mitano.

Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47, leo imelazimishwa sare na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba inaonekana kuimarika tangu kocha huyo alipotwaa mikoba ya Joseph Omog ambaye mkataba wake ulivunjwa baada ya vigogo hao kuondolewa Kombe la Azam.

Tangu Lechantre alipoanza kazi wachezaji Aishi Manula, Shomary Kapombe, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Emmanuel Okwi, John Bocco na Said Ndemla wamejihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.

Simba inashuka kwenye uwanja wa Taifa kesho Alhamisi kuikabili Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 23.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →