Okwi anahitaji mabao 5 kuvunja rekodi za Tambwe, Kiiza

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Apr 2018
Okwi anahitaji mabao 5 kuvunja rekodi za Tambwe, Kiiza
Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi amefunga goli lake la 17 la ligi kuu Tanzania bara msimu huu wakati Simba ikipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ushindi ambao unaiongezea Simba matumaini ya kushinda taji la VPL.

Okwi tayari ameshaivunja rekodi ya wafungaji bora wa msimu uliopita 2016/17 (Simon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Musa (Ruvu Shooting) ambao kila mmoja alifunga magoli 14 katika msimu huo. Okwi aliivunja rekodi hiyo Februari 26, 2018 baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Mbao ambapo Simba ilishinda 5-0 ligi ikiwa mzunguko wa 19.

Kwa sasa Okwi anaifukuzia rekodi ya mganda mwenzake Hamis Kiiza ambaye alifunga magoli 19 msimu wa 2015/16 na kuwa mfungaji bora wa klabu ya Simba kwa msimuo. Rekodi nyingine anayoikimbiza ni ya Amis Tambwe mfungaji bora wa msimu wa 2015/16 ambaye alifunga magolki 21.

Okwi amebakiza magoli mawili kuifikia rekodi ya Kiiza ndani ya Simba huku akiwa anahitaji magoli matano ili kuivunja rekodi ya Tambwe mfungaji bora wa misimu wili iliyopita.

Simba imebakiza mechi nane za ligi ligi kuu, Okwi ana rekodi nzuri ya kufunga magoli mengi kwenye viwanja vya Dar (Uhuru na uwanja wa taifa) katika mechi nane ambazo zimebaki, Simba itacheza mechi tano nyumbani, kutokana na rekodi ya Okwi kwenye viwanja Dar huenda akazifikia rekodi hizo na kuzivunja.

ShaffihDaudi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’