FT : Mtibwa Sugar 0-1 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Apr 2018
FT : Mtibwa Sugar 0-1 Simba
Wekundu wa Msimbazi, Simba wameongeza kasi kuelekea ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuilaza Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

Ikiungwa mkono na idadi kubwa ya mashabiki wake waliosafiri kutoka maeneo ya jirani ya mkoa wa Morogoro, Simba iliandika bao lake kwenye dakika ya 23 mfungaji akiwa Emanuel Okwi aliyeunganisha vyema pasi ya kichwa aliyotengewa na John Bocco.

Changamoto ya hali ya uwanja uliojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro, ilichangia kwa kiasi kikubwa kwa timu zote kushindwa kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wengi waliofurika uwanjani hapo.

Mtibwa Sugar iliyokuwa nyumbani ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini uimara wa mlinda lango wa Simba Aishi Manula uliwawezesha vinara hao wa ligi kuondoka na alama zote tatu muhimu.

Matokeo hayo yanazidi kuisogeza Simba karibu na ubingwa sasa ikiongoza kwa tofauti ya alama sita baada ya kufikisha alama 52.

Kinara wa mabao, Emanuel Okwi ameendelea kuwaacha wapinzani wake kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu, kwani sasa amefikisha mabao 17.

John Bocco na Obrey Chirwa ndio wanaomfuatia kwa karibu wote wakiwa wamefunga mabao 12 kila mmoja
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’