TFF imependekeza Wambura ashitakiwe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Apr 2018
TFF imependekeza Wambura ashitakiwe
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura huenda akafikishwa mbele ya vyombo vya sheria baada ya juzi Kamati ya Rufaa za Maadili ya shirikisho hilo kupendekeza hivyo wakati ikitupa rufaa yake aliyokata kupinga adhabu ya kufungiwa maisha kujishughulisha na mchezo huo iliyokuwa inamkabili.

Machi 15 mwaka huu, Wambura, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF) alikata rufaa kwa kamati hiyo iliyoko chini ya Wakili Ebenezer Mshana kupinga hukumu ya kufungiwa maisha iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.

Mwenyekiti huyo wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) alikutwa na hatia katika makosa matatu aliyokuwa anatuhumiwa ambayo ni kupokea malipo ambayo hayakuwa halali, kughushi barua kutoka kwa Kampuni ya Jeck's na kushusha hadhi ya shirikisho kwa kuzingatia kifungu cha 73 (1) cha Kanuni za Maadili za TFF .

Wakili Mshana alisema kuwa kamati yake imeamua kuitupilia mbali rufaa hiyo ya Wambura kwa sababu ya ukubwa wa kesi iliyokuwa inamkabili na kueleza kuwa mawakili wa mrufani walikuwa wakijitika zaidi kiufundi badala ya kwenda kwenye hoja za msingi.

Wakili Mshana alisema kuwa waliamua adhabu hiyo iendelee na hatua zaidi za kisheria kuchukua mkondo wake baada ya kujiridhisha na ushahidi uliofikishwa katika kamati yake ambao ni pamoja na ripoti ya ukaguzi wa fedha iliyofanywa na Kampuni ya nje iitwayo TAC.

"Ripoti inaonyesha kampuni iliyokuwa inamilikiwa na Michael Wambura ndio ilikuwa wasambazaji wakuu wa thamani za hosteli na pia aliwahi kukiuka kanuni za michezo huo za TFF na Fifa kwa kupeleka shughuli za soka mahakamani...inaonyesha aliipeleka Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akifungua kesi namba 100 ya mwaka 2010," alisema Wakili Mshana.

Aliongeza kuwa adhabu iliyotolewa ilikuwa ni sahihi kwa nafasi yake na akisisitiza kuwa Wambura alikuwa anaifahamu kesi hiyo kwa kufuatilia mwenendo mzima kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka huu ambapo alifikishwa katika Kamati ya Maadili.

Wakati huo huo kamati hiyo ya Wakili Mshana imependekeza Mkuu wa Kituo cha Soka cha Mtwara, Dustan Mkundi, kufikishwa katika vyombo vya sheria baada ya kuchelewa kuwasilisha fomu ya mapato katika muda uliowekwa kikanuni wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Ndanda FC dhidi ya Simba iliyofanyika Desemba 20 mwaka jana.

Edgar Chibura, Mwenyekiti wa timu ya Abdajalo ya jijini ameshinda rufani yake aliyokata kupinga adhabu ya kufungiwa kujishughulisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja na kulipa faini ya Sh. milioni tatu.

Katika rufani hiyo, Wambura alikuwa anatetewa na mawakili watatu wakiwamo Dk, Masumbuko Lamwai na Emmanuel Muga ambaye aliomba mteja wake apunguziwe adhabu kutoka kifungo cha maisha na kuwa angalau miaka mitano.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’