Mlinzi wa kati wa Simba Salim Mbonde amerejea katika kikosi cha Simba ambacho kiko mkoani Morogoro kikijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar keshokutwa Jumatatu.
Mbonde aliumia kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji lakini ni habari njema kwamba alipata maumivu ya kawaida na hakuwa ametonesha jeraha lake la goti kama ilivyokuwa imedhaniwa awali.
Kurejea kwake kikosini kinampa ahueni kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre ambaye atawakosa wachezaji wake watatu muhimu kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
James Kotei, Erasto Nyoni na Juuko Murshidi watakosekana kwenye mchezo huo kwa kuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano kila mmoja.
Mbonde atakuwa na nafasi ya kuwakabili waajiri wake wa zamani, Mtibwa Sugar.
Aidha, kukosekana kwa wachezaji hao watatu hakumpi hofu Lechantre ambaye ametamba kuwa wapo wachezaji watakaoziba nafasi zao kikamilifu.
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 49, alama tatu zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili. Ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar utaifanya ijiimarishe zaidi kileleni.

ADVERTISE HERE