Ni muujiza pekee utakaoikosesha Simba ubingwa msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Apr 2018
Ni muujiza pekee utakaoikosesha Simba ubingwa msimu huu
Mbio za ubingwa zimeshika kasi kwa Simba, Yanga na Azam kila moja inapiga hesabu kali za kuwania ubingwa huo misimu huu.

Katika mbio za ubingwa Simba inaongoza kwa pointi 49, wakifuatiwa na Yanga (46) na Azam (44), ndio timu zenye nafasi kubwa ya kugombania ubingwa kutokana na gepu kuwa dogo la pointi.

Huu hapa uchambuzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti la Mwanaspoti ambao unaipa Simba nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kuliko Yanga na Azam FC

KIKOSI KIPANA

Inawezekana hivi sasa Simba ndio timu yenye kikosi kipana zaidi kuliko kikosi chochote katika ligi msimu huu.

Simba wana wachezaji wengi wenye uwezo, ambapo hata akikosekana mchezaji wa kikosi cha kwanza, basi pengo lake litazibwa vizuri.

Hii inaonyesha dhahiri kwamba walishapanga mapema kwamba msimu huu lazima wapambane kuhakikisha wanachukua ubingwa baada ya kulikosa kwa muda mrefu.

HAWANA MAJERUHI WENGI

Tumeona Azam wakihaha na wachezaji wao majeruhi katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mechi zao.

Anapoumia mchezaji wa kikosi cha kwanza wanakuwa katika kipindi kigumu, tumeona hilo kwa Mbaraka Yusuph na hata Himid Mao alivyoumia.

Yanga nao vile vile licha ya kushika nafasi ya pili, lakini wachezaji wao nyota walivyokosekana ndio wamezidi kwenda mwendo wa kuchechemea chechemea.

Simba kwao majeruhi wengi wanaotokea siyo wa kikosi cha kwanza, kikosi cha kwanza akiumia hakai nje muda mrefu anarejea, hivyo hii itasaidia kuendeleza spidi yao ya ushindi wao.

MOTISHA

Suala la ukata kwao hawalijui kabisa yani. Msimu huu wana Tajiri wao Mohammed Dewji ambaye anataka timu ifanye vizuri hivyo huwa anawapa bonusi katika kila mchezo.

Hii inaongeza morali kwa wachezaji kwasababu wanajua kwamba tunatakiwa tufanye vizuri ili tuisaidie timu, lakimi vile vile tusimuangushe bosi wetu anayetuunga mkono.

Suala hili kwa Yanga ni zito kutokana na ukata walionao, lakini kwa upande wa Azam uwezo wanao mkubwa lakini wanaonekana wamejitoa wenyewe katika mbio za kusaka ubingwa licha ya kwamba wanaweza kufanya maajabu.

WAMEBAKI LIGI KUU TU

Baada ya kutolewa na Al Masry, akili yao waliigeuzia katika ligi kuu tu na sio kitu kingine, hii ni kutokana walishatolewa mapema katika Kombe la Azam Federation Cup.

Yanga hivi sasa wamekuwa kama fisi anayefuata mkono wa binadamu, akitegemea udondoke ili ale kwa sababu hajui ataponea wapi mpaka dakika hii.

Bado anataka afuzu katika hatua ya mbele zaidi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, huku akiutaka ubingwa wa Ligi Kuu, wakati wenzao wao wanaangalia tu ligi, hivyo Simba wanakila sababu ya kubeba ndoo labda washindwe wenyewe tu.

OKWI, BOCCO HATARI

Unaweza ukawaita waziri wa mambo ya ndani na mwingine waziri wa mambo ya nje.

Emmanuel Okwi yeye anafunga ndani Dar es Salaam wakati John Bocco anafunga nje mikoni, sasa hapo unategemea Simba itafanya vibaya?

Klabu hii katika orodha ya wafungaji kuna mchezaji wao Emmanuel Okwi, mpaka hivi sasa ana mabao 16, anafuata Bocco ana mabao 12, ambaye amefungana na Obrey Chirwa wa Yanga mwenye magoli 12.

Kwa spidi ya Okwi na Bocco msimu huu ndio inachangia kujiweka zaidi katika ubingwa kwa sababu wameshaifungia timu hiyo mabao 28 katika ligi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’