Kichuya ni moja ya 'Engine' muhimu za Simba

Shabiki Waukweli By Shabiki Waukweli
β€’
25 Sep 2017
Kichuya ni moja ya 'Engine' muhimu za Simba
Shiza Ramadhani Kichuya ni mmoja wa washambuliaji wa pembeni ambaye ana kipaji cha hali ya juu. Uchezaji wake unaweza kuufananisha na ule wa winga wa zamani wa Yanga na Stars, Edibily Lunyamila.

Uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kuwatoka walinzi kwa kasi umemfanya awe tofauti sana na washambuliaji wengi wa Tanzania.

Licha ya kuwa na kikosi kipana chenye kila aina ya mchezaji, Shiza Kichuya na Emanuel Okwi hawa ndio wachezaji ambao uwepo wao dimbani utaibeba sana Simba msimu huu.

Kichuya tayari amefunga mabao mawili kwenye ligi msimu huu na mwenyewe amesisitiza anakitaka kiatu cha dhahabu licha ya kwamba bado ana kazi ya kumfikia 'Mnyama' Okwi mwenye mabao sita tayari.

Kwenye mchezo dhidi ya Mbao kichuya alipata majeraha katika kisigino chake lakini tayari ameshaanza mazoezi mepesi.

Mkuu wa Kitengo cha habari cha Simba, Haji Manara amesema atakuwa tayari kushuka dimbani kwenye mchezo ujao dhidi ya Stand United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’